Jumamosi, 28 Juni 2014

VUNJIKA MBAVU NA KING MAJUTO NDANI YA FILAMU YA INSIDE

Filamu hii Jennifer Kyaka (Odama) ambayo inayonyesha maisha ya wafanyakazi maofisi wanaovyofanya vituko na mabosi wao na wengine hata kumkufuru na kumuudhi Mungu kwa vitendo vya rushwa na uvivu kazini, kwa mana Mungu amesema asiyefanya kazi na asile. Watu badala ya kufanya kazi wanabaki kupiga stori na majungu maofisi. Wadada wanavyotumia uzuri wao kuwalaghai waume za watu kwa kutoa rushwa ya ngono. Hakika kama mcha Mungu ndani ya hii filamu utajifunza mengi na utaburudika na vituko vya wasanii maarufu wa kuchekesha kama KING MAJUTO na  BENY, pia utamuona marehemu RACHEL HAULE, DAVINA, ODAMA, DULLAH WA PLANET BONGO, na wengine wemgi sana. Filamu hii ambayo imetengezwa na kampuni bora Tanzania ya J-FILM 4 LIFE itakuweka mahali fulani KIMAWAZO.

Jumanne, 15 Aprili 2014

MTU NA KAKA YAKE, GRACE NA JOSHU KUACHIA ALBAMU YAO YA KWANZA YA MY SAVIOUR GOD

Baada ya kumtumikia Mungu kwa njia mbalimbali, Grace na Joshu wameamua sasa kumuimbia Mungu na kumtukuza ili Mungu mwenyewe ajitwalie utukufu. Waimbaji hawa ni ndugu (ni mtu na mdogo wake). Baada ya Bwana Joshu kuona ana kitu ndani yake cha kumtukuza Mungu aliamua kumjulisha dada yake Grace Christian Rwegasha kwamba anahisi kumuimbia Mungu na wakati umeshafika, Grace alikubaliana na wakaamua kuingi studio na kufanya albamu yao hii ya kwanza.

Grace Christian Rwegasha

Grace anasema kwake ni mara ya kwanza kufanya huduma ya uimbaji ni alipata wakati mgumu sana wa kuamua kuanza kuimba kwani alikuwa hajajipanga kwa kazi hii ya Bwana. Ila alisema hali ya kumuimba alikuwa nayo moyoni tangia muda mrefu sana lakini hakufikiria kwamba atakuja kuingia studio na kufanya kama alivyofanya siku ya leo. Garce alisema katika uimbaji wake anapata ugumu sana kuimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili  ila anapoimba kwa lugha ya Kiingereza anajisikia huru zaidi na ukiangalia albamu yao nusu ni nyimbo za Kiswahili na nusu ni nyimbo za Kiingereza.

Grace Christian Rwegasha
Ukisikiliza nyimbo zao hakika utatambua ya kwamba waimbaji hawa wamekuja kufanya mapinduzi ya muziki wa Injili Tanzania, kuna vitu vya kipekee ambavyo huwezi kusikia kwa waimbaji wengine wanavyotumia katika huduma yao  ya uimbaji.

Grace Christian Rwegasha
Joshua (Joshu) ni kijana ambaye amekuwa mtundu sana katika eneo la muziki kwa muda mrefu sana, na sasa yuko Mwanza kimasomo katika chuo cha St. Agastine. Amekuwa akitamani sana muziki na ikafikia kipindi anatengeneza biti za muziki na kuimba. Kuna baadhi ya nyimbo alizoimba katika albamu hii ametengeneza biti yeye mwenyewe. Kwa sasa Joshu yuko Mwanza kimasomo na dada yake Grace yupo hapa Dar es Salaam.

Grace Christian Rwegasha
Waimbaji waliomba sana watu wawapokee kwani ndio wameanza kufanya kazi ya Mungu na pia waliwaomba watu wa media kuonyesha ushirikiano wao katika kupiga nyimbo zao na kufanya mahojiano ili watu waweze kujua ya kwamba kuna kitu kipya Mungu anatumia kwa kazi yake. Pia aliomba ushirikiano na watumishi wa Mungu katika huduma zao na matamsha yao kuwashirikisha

Rumafrica iko katika maandalizi ya kutengeneza DVD yao ya maohojiano ambayo utasikia katika Youtube, Facebook na katika blogu hii na blogu mbalimbali.

Grace na Joshu wamesema wako tayari kufanya kazi ya Mungu mahali popote na wakati wowote kwani wameojitambua ya kwamba wameitwa na Mungu kufanya kazi  ya Bwana.

Mbali na uimbaji, Rumafrica iliona kuna kitu ambacho watumishi hawa wanacho hasa katika kuhubiri na kutoa ushauri. Utakuja kujua haya utakaposikia mahojiano yetu.

Unaweza kuwasiliana na Grace kwa simu +255 788 443 346 au +255 654 407080

MUNGU AKUBARIKI

Ijumaa, 27 Septemba 2013

TINA SOAP KWA KUOSHEA MAGARI, TILES< CHOONI, MASINK N.K INAPATIKANA

JIPATIE TINA SOAP KUTOKA KWA MTANGAZAJI WA PRAISE POWER-CHRISTINA MTU

TINA SOAP ni sabuni  nzuri sana kwa matumizi ya kuoshea magari, tiles, bafuni, chooni, masink, jikoni na sehemu mbalimbali ili kuangamiza wadudu kama vile mende, inzi, sisimizi n.k
Jipatie sasa kulinda afya yako...!!!

Sticker zimetengenezwa na RUMAFRICA +255 715851523

Mtangazaji wa Praise Power Radio, Christina Mtua akiwa katika ofisi ya Rumafrica Sinza Afrikasana hapa jini DSM

Jumatatu, 16 Septemba 2013

STELLA JOEL ASHANGAZA WALIO WENGI KATIKA HARUSI YAKE SIKU YA JUMAMOSI


PICHA ZIMEPIGWA NA RUMAFRICA +255 715851523

Mungu ni mwema na ni Mungu wa vitendo. Baada ya maombezi makali ya kila mtu kumtafuta yule ampendae, Mungu aliweza kujibu kilio cha Stella Joel na mpenzi wake Yerimo kwa kufanikisha ndoa yao iliyofungwa katika kanisa la Pentecostal Holiness Mission Light House Christian Center Ubungo na tafrija kufanyika katika ukumbi wa Mawasiliano Ubungo jijini Dar esa Salaam siku ya jumamosi

UNAWEZA KUWASILIANA NA STELLA JOEL KWA SIMU HII  +255 756 846166
AU +255715 049143


Stella Joel kutoka Bukoba (Mhaya)

Yerimo kutoka Iringa (Mhehe)

Bloga wenu Rulea Sanga aliyehusika ipasavyo kukuletea habari hizi na kupiga picha

MATUKIO KATIKA PICHA
SEHEMU YA KWANZA

WAKIANDAA SURA ZAO NA MAVAZI YAO

STELLA JOEL AKIELEKEA KANISANI AKITOKEA SALOON

Mwimbaji wa nyimbo za injili Madam Rutiu ndiye aliyekuwa dereva wa Bwana na Bibi Harusi


MAENEO YA KANISANI

WAZAZI WAKIMRUSHU BIBIU HARUSI KUPOKELEWA NA BWANA HARUSI KANISANIKulia ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Orida Njole


Kulia ni mwimbaji wa nyimbo za injili, Janet Mrema
Mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania, John Shabani


Mchungaji Mwasota
Mchungaji Mwasota akiangalia pete kwa makini kabla hajawakabidhi Bwana Harusi na Bibi Harusi kuvishanav
KIPINDI CHA KUMPONGEZA MAHARUSI BAADA YA KUVISHANA PETE NA KUSAINI

Mdogo wake na Stell Joel (kulia)


KIPINDI CHA KUFUNGA IBADA-KANISANI
WAKATI WA KUELEKEA UKUMBINI ULIFIKA NA SASA SAFARI IMEANZA


 MATUKIO YA UKUMBINI ENDELEA KUTEMBELEA BLOGU HII

MUNGU WANGU NA AKUBARIKI SANA


KAMA UNAHITAJI HUDUMA YA PICHA WASILIANA NAMI KWA SIMU +255 715 851523


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...