Filamu
hii Jennifer Kyaka (Odama) ambayo inayonyesha maisha ya wafanyakazi
maofisi wanaovyofanya vituko na mabosi wao na wengine hata kumkufuru na
kumuudhi Mungu kwa vitendo vya rushwa na uvivu kazini, kwa mana Mungu
amesema asiyefanya kazi na asile. Watu badala ya kufanya kazi wanabaki
kupiga stori na majungu maofisi. Wadada wanavyotumia uzuri wao
kuwalaghai waume za watu kwa kutoa rushwa ya ngono. Hakika kama mcha
Mungu ndani ya hii filamu utajifunza mengi na utaburudika na vituko vya
wasanii maarufu wa kuchekesha kama KING MAJUTO na BENY, pia utamuona
marehemu RACHEL HAULE, DAVINA, ODAMA, DULLAH WA PLANET BONGO, na wengine
wemgi sana. Filamu hii ambayo imetengezwa na kampuni bora Tanzania ya
J-FILM 4 LIFE itakuweka mahali fulani KIMAWAZO.
Jumamosi, 28 Juni 2014
Jumanne, 15 Aprili 2014
MTU NA KAKA YAKE, GRACE NA JOSHU KUACHIA ALBAMU YAO YA KWANZA YA MY SAVIOUR GOD
Baada
ya kumtumikia Mungu kwa njia mbalimbali, Grace na Joshu wameamua sasa
kumuimbia Mungu na kumtukuza ili Mungu mwenyewe ajitwalie utukufu.
Waimbaji hawa ni ndugu (ni mtu na mdogo wake). Baada ya Bwana Joshu
kuona ana kitu ndani yake cha kumtukuza Mungu aliamua kumjulisha dada
yake Grace Christian Rwegasha kwamba anahisi kumuimbia Mungu na wakati
umeshafika, Grace alikubaliana na wakaamua kuingi studio na kufanya
albamu yao hii ya kwanza.
Grace Christian Rwegasha
Grace anasema kwake ni mara ya kwanza kufanya huduma ya uimbaji ni alipata wakati mgumu sana wa kuamua kuanza kuimba kwani alikuwa hajajipanga kwa kazi hii ya Bwana. Ila alisema hali ya kumuimba alikuwa nayo moyoni tangia muda mrefu sana lakini hakufikiria kwamba atakuja kuingia studio na kufanya kama alivyofanya siku ya leo. Garce alisema katika uimbaji wake anapata ugumu sana kuimba kwa kutumia lugha ya Kiswahili ila anapoimba kwa lugha ya Kiingereza anajisikia huru zaidi na ukiangalia albamu yao nusu ni nyimbo za Kiswahili na nusu ni nyimbo za Kiingereza.
Grace Christian Rwegasha
Ukisikiliza nyimbo zao hakika utatambua ya kwamba waimbaji hawa wamekuja kufanya mapinduzi ya muziki wa Injili Tanzania, kuna vitu vya kipekee ambavyo huwezi kusikia kwa waimbaji wengine wanavyotumia katika huduma yao ya uimbaji.
Grace Christian Rwegasha
Joshua (Joshu) ni kijana ambaye amekuwa mtundu sana katika eneo la muziki kwa muda mrefu sana, na sasa yuko Mwanza kimasomo katika chuo cha St. Agastine. Amekuwa akitamani sana muziki na ikafikia kipindi anatengeneza biti za muziki na kuimba. Kuna baadhi ya nyimbo alizoimba katika albamu hii ametengeneza biti yeye mwenyewe. Kwa sasa Joshu yuko Mwanza kimasomo na dada yake Grace yupo hapa Dar es Salaam.
Grace Christian Rwegasha
Waimbaji waliomba sana watu wawapokee kwani ndio wameanza kufanya kazi ya Mungu na pia waliwaomba watu wa media kuonyesha ushirikiano wao katika kupiga nyimbo zao na kufanya mahojiano ili watu waweze kujua ya kwamba kuna kitu kipya Mungu anatumia kwa kazi yake. Pia aliomba ushirikiano na watumishi wa Mungu katika huduma zao na matamsha yao kuwashirikisha
Rumafrica iko katika maandalizi ya kutengeneza DVD yao ya maohojiano ambayo utasikia katika Youtube, Facebook na katika blogu hii na blogu mbalimbali.
Grace na Joshu wamesema wako tayari kufanya kazi ya Mungu mahali popote na wakati wowote kwani wameojitambua ya kwamba wameitwa na Mungu kufanya kazi ya Bwana.
Mbali na uimbaji, Rumafrica iliona kuna kitu ambacho watumishi hawa wanacho hasa katika kuhubiri na kutoa ushauri. Utakuja kujua haya utakaposikia mahojiano yetu.
Unaweza kuwasiliana na Grace kwa simu +255 788 443 346 au +255 654 407080
MUNGU AKUBARIKI

Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)